Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Haki za binadamu

Wakimbizi wa Sudan wawasili katika mji wa mpaka wa Adre nchini Chad.
© UNHCR/Andrew McConnell

Vita Sudan yasababisha ongezeko la wakimbizi, UNHCR yataka msaada wa haraka

“Machafuko yasiyokoma nchini Sudan yamesababisha mgogoro mkubwa zaidi wa usalama kwa raia kwa miongo kadhaa, huku zaidi ya watu milioni 3 wakilazimika kukimbia nchi hiyo tangu vita ilipoanza miezi 19 iliyopita.” Dominique Hyde, Mkurugenzi wa Uhusiano wa Nje wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) amesema hayo leo jijini Geneva, USwisi akizungumza na waandishi wa habari.

Mizozo na ukosefu wa utulivu vinaweza kuchochea viwango vya juu vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto, wanawake na wasichana
© UNICEF/STARS/Kristian Buus

Nchi zaahidi kuondokana na ukatili dhidi ya watoto ikiwemo adhabu ya viboko

Uganda na Burundi ni miongoni mwa nchi zaidi ya 100 duniani zilizochukua hatua ya kihistoria kuahidi kumaliza ukatili dhidi ya watoto, ikiwemo kupiga marufuku adhabu ya viboko, suala linaloathiri watoto 3 kati ya 5 majumbani mwao. Ahadi hizi zimetolewa katika mkutano muhimu uliofanyika Bogotá, Colombia, unaolenga kukubaliana juu ya tamko jipya la kimataifa la kuwalinda watoto dhidi ya aina zote za ukatili, unyonyaji, na dhuluma.

Katibu Mkuu wa UN António  Guterres akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea Bucha, Ukraine Aprili, 28 2022. (MAKTABA)
UN Photo/Eskinder Debebe

Kutohukumu uhalifu dhidi ya wanahabari ni ‘tanuri’ la ghasia - Guterres

Mkataba wa Zama Zijazo uliopitishwa mwezi uliopita unataka waandishi wa habari na wale wanaoambatana nao wakati wanafanya kazi zao katika maeneo ya mizozo, sio tu waheshimiwe bali pia walindwe, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres katika ujumbe wake leo hii Novemba 2, ambayo ni siku ya kimataifa ya kupinga ukwepaji sheria kwa uhalifu dhidi ya wanahabari.

Alice Nderitu, Mshauri Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uzuiaji wa mauaji ya kimbari
Kate McElwee

Hali ya Mashariki ya Kati, Alice Wairimu Nderitu atoa kauli

Mshauri Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Kuzuia Mauaji ya Kimbari, Alice Wairimu Nderitu, leo Oktoba 29 ametoa wito wa kutanguliza juhudi zote zinazowezekana za kidiplomasia ili kukomesha uhasama unaoendelea Mashariki ya Kati na kuongeza maradufu juhudi zote za kuimarisha ulinzi wa raia wasio na hatia, na vile vile kuhakikisha uwasilishaji wa misaada muhimu ya kibinadamu kwa watu wenye uhitaji zaidi.