Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Tabianchi na mazingira

Watoto wakifanya kazi kwenye migodi Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
© UNICEF/Patrick Brown

Mpito wa nishati haupaswi kuchochea hila na ubinafsi unaokandamiza maskini: COP29

Mkutano wa Umoja  wa Mataiifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 ulioingia siku ya tatu leo huko Baku Azerbaijan leo umegeukia suala kubwa la jinsi ya kudhibiti mahitaji ya madini muhimu kwa ajili ya kutengeneza magari ya umeme na paneli za nishati ya jua au sola bila kuibua "mkanyagano wa hila ambao unakandamiza jamii za wenyeji na kuchochea maskini.”

Patricial Kombo Mumbua kutoka Kenya, mmoja wa washiriki wa mkutano wa COP29 Baku.
UN News

Ufadhili wa fedha utakuwa jawabu mujarabu kudhibiti mabadiliko ya tabianchi Afrika: Mshiriki Patricia Kombo

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 leo ukiingia siku ya nne  mjini Baku Azerbaijan vijana kutoka Afrika wataka ufadhili uongezwe kutoka mataifa makubwa hususan yanayochangia zaidi hewa ukaa ili kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi kwa mataifa yanayoendelea ambapomiongoni mwa waathirika wakubwa ni vijana.

Sauti
1'51"
Miaka ya mafuriko yamesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao na kubaki bila makazi huko Bentiu, Sudan Kusini. (faili)
© UNHCR/Andrew McConnell

UNHCR Sudan Kusini yachukua hatua kupunguza madhara ya mafuriko kwenye kilimo

Huko Maban, jimboni Upper Nile, kaskazini mashariki mwa Sudan Kusini, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi ,UNHCR linajenga vifaa vya kuhifadhi maji pamoja na makinga maji ili kuepusha mashamba dhidi ya mafuriko ya msimu yanayokumba eneo hilo mara kwa mara, eneo ambalo ardhi yake ina rutuba kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara. 

Sauti
2'12"
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kushoto) akihutubia mkutano wa COP29 mjini Baku, Azerbaijan.
UN Climate Change/Kiara Worth

Tusipolipa gharama ya mabadiliko ya tabianchi sasa ubinadamu utalipa gharama hiyo aonya Guterres kwenye COP29

Leo katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP29, ulioandaliwa katika mji mkuu wa Azerbaijan,a kuanza jana tarehe 11-22 Novemba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema kwamba viongozi waliokusanyika Baku kwa Mkutano wa 29 wa utekelezaji wa mabadiliko ya tabianchi au COP29 lazima wachukue hatua za haraka kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa, kuwalinda watu kutokana na mabadiliko ya tabianchi, na kutatua changamoto za ufadhili dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ili kukabiliana na janga hilo kubwa na athari zake ambazo ulimwengu umezishuhudia mwaka 2024.

Mafuriko makubwa yameathiri wakimbizi wa Cameroon katika eneo la wakimbizi la Guilmey nchini Chad.
© UNHCR/Andrew McConnell

Kando ya vitisho vya usalama, wakimbizi wakabiliwa pia na madhara ya mabadiliko ya tabianchi

Huku dunia ikizidi kutafuta suluhu ya changamoto zinazoletwa na mabadiliko ya tabianchi, watu waliolazimika kukimbia vita, vurugu na mateso wanajikuta kwenye mstari wa mbele wa janga la mabadiliko ya tabianchi. Imesema ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) iliyotolewa leo wakati mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa  mabadiliko ya tabianchi, COP29  ukiendelea huko Baku, Azerbaijan.