Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Afya

Chanjo ya Malaria ilitolewa kwa mara ya kwanza nchini Sudan katika juhudi za kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa huo hatari.
© UNICEF/Ahmed Mohamdeen Elfatih

Sudan imeanza kutoa chanjo dhidi ya Malaria kwa watoto

Wizara ya Afya ya Sudan kwa kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa, imetangaza uzinduzi wa chanjo ya kwanza ya malaria nchini humo, ikiwa ni jitihada za kulinda watoto dhidi ya ugonjwa huu unaoleta madhara makubwa kwa afya. Chanjo hii imeanza kutolewa katika vituo vya afya katika maeneo ya Gedaref na Blue Nile, ambapo watoto wapatao 148,000 wenye umri wa chini ya mwaka mmoja wanatarajiwa kunufaika.