Vichwa vya Habari
Habari Moto Moto
Chaguo la Mhariri
Makala Maalum
Utamaduni na Elimu
Huko Havana Cuba Kongamano la kimataifa la Kiswahili limekunja jamvi mwishoni mwa wiki ambapo wadau kutoka nchi mbalimbali kuanzia barani Ulaya, Marekani kaskazini na Kusini, Asia na wenyeji Afrika walikutana na kujadili jinsi ya kukuza lugha ya Kiswahili duniani sanjari na kutekeleza malengo ya Umoja wa Mataifa kama kutumia Kiswahili kudumisha amani na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs.
Habari kwa Picha
Mkuu wa UN asema UNRWA haina mbadala
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametangaza kuwa hakuna mbadala wa Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa wa Kipalestina UNRWA, ambalo limekuwa likichangia ustawi na maendeleo yao tangu mwaka 1950.
Wakati huo huo, Kamishna Mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini amesisitiza kwamba miswada ya Israel ya kusitisha operesheni za shirika hilo si kitu kidogo bali ni adhabu ya pamoja.
Habari Nyinginezo
Tabianchi na mazingira
Je mnataka bei za vyakula na nishati iongezeke zaidi?
Je mnataka nchi zenu ziendele kushindwa kushindana kiuchumi?
Je mnataka dunia yetu iendelee kukosa utulivu na kugharimu maisha adhimu ya binadamu?
Afya
Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa kuchagiza kaya kulima bustani za mboga za majani pamoja na ufugaji wa kuku huko jimbo la Afar, kaskazini mashariki mwa Ethiopia umesaidia familia za vijijini kukabiliana na utapiamlo miongoni mwa watoto.