Kando ya vitisho vya usalama, wakimbizi wakabiliwa pia na madhara ya mabadiliko ya tabianchi
Huku dunia ikizidi kutafuta suluhu ya changamoto zinazoletwa na mabadiliko ya tabianchi, watu waliolazimika kukimbia vita, vurugu na mateso wanajikuta kwenye mstari wa mbele wa janga la mabadiliko ya tabianchi. Imesema ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) iliyotolewa leo wakati mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 ukiendelea huko Baku, Azerbaijan.