Nenda kwa yaliyomo

Kifausi (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyota za kundinyota Kifausi (Cepheus) katika sehemu yao ya angani (nyota karibu zaidi na ncha ya anga hazionekani kutoka Afrika ya Mashariki)
Ramani ya Kifausi (Cepheus), kwa macho ya mtazamaji kwenye nusutufe ya kaskazini
Nyota za kundinyota Kifausi (Cepheus) jinsi ilivyochorwa miaka 200 iliyopita pale Ulaya


Kifausi (Cepheus kwa Kilatini na Kiingereza) [1]. ni jina la kundinyota kwenye angakaskazi ya dunia yetu.

Mahali pake

Kifausi ni kundinyota kubwa karibu na ncha ya anga ya kaskazini na nyota zake za kusini zinaonekana pia katika Afrika ya Mashariki.

Inapakana na makundinyota jirani ya Dajaja (Cygnus), Mjusi (Lacerta), Mke wa Kurusi (Cassiopeia), Twiga (Camelopardalis) na Dubu Mdogo (Ursa Minor)

Jina

Kifausi lilijulikana kwa jina hili kwa miaka mingi na mabaharia Waswahili walioitumia kupata njia baharini wakati wa usiku.[2]

Jina la Kifausi linatokana na Kiarabu قِيفاوس qiifaaws ambayo ni umbo la jina asilia la Kigiriki Κηφεύς Kefeus (baadaye Cepheus kwa tahajia ya Kilatini).

Katika mitholojia ya Ugiriki ya Kale alikuwa mfalme wa Ethiopia na mume wa malkia Cassiopeia (Mke wa Kurusi) aliyejivunia kuwa yeye mwenyewe na binti yake Mara (Andromeda) ni wazuri kushinda mabinti wa Poseidon mungu wa bahari. Hapo Poseidon aliamua kumwadhibu kwa kutuma dubwana Ketusi dhidi yake. Kifausi pamoja na malkia yake waliamua kumtoa binti Mara (Andromeda) kama sadaka kwa Ketusi kwa kumfunga kwenye ufuko wa bahari ili aliwe na dubwana huyu lakini shujaa Farisi (Perseus) akaingia kati na kumwokoa. Baadaye wote waliinuliwa angani kama nyota [3] kwa hiyo tunaona Kifausi (Cepheus) jirani na kundinyota za Mke wa Kurusi (Cassiopeia) na Mara, halafu Ketusi na Farisi aliyekuja kumwokoa Mara katika simulizi la mitholojia.

Kifausi ni kati ya makundinyota yaliyotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika karne ya 2 BK kwa jina Kassiopeia. Iko pia katika orodha ya makundinyota 88 ya Umoja wa kimataifa wa astronomia [4] kwa jina la Cepheus. Kifupi chake rasmi kufuatana na UKIA ni 'Cep'.[5]

Nyota

Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miakanuru)
Aina ya spektra
α 5 Alderamin 2,45 0049 A7 IV-V
β 8 Alfirk 3,15 - 3,21 ca. 700 B2 III
γ 35 Errai, Arrai, Alrari 3,22 0046 K1 IV
ζ 21 Tsao Fu 3,39 0726,43 K1 Ib
η 3 Eta Cephei 3,40 0046,78 K0 IV
ι 32 Iota Cephei 3,50 0115,38 K1 III
δ 27 Al Radif, Delta Cephei 3,6 - 4,3 0950,92 F5 - G3 Ib
μ Erakis 3,62 - 5,0 5260,73 M2 Iab + M0 + A
ε 23 Phicares 4,18 0083,93 F0 IV
θ 2 Al Kidr 4,20 0135,68 A7 III
ν 10 Cor Regis 4,25 5096,36 A2 Ia
ξ 17 Alkurah, Kurah 4,26 0085,83 A3 + F7

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Cepheus" katika lugha ya Kilatini ni " Cephei " na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Cephei, nk.
  2. ling. Knappert 1993
  3. ling. Allen, Star-Names and their Meanings uk, 117
  4. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  5. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy. 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R.


Marejeo

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 75 ff (online hapa kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kifausi (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.