York ni mji wa Ufalme wa Maungano ulioko kaskazini mwa Uingereza, kando ya mto Ouse (Yorkshire).

Kitovu cha kihistoria cha York.

Hutazamwa kama makao makuu ya Yorkshire ingawa kiutawala si sehemu ya Yorkshire tena, bali eneo la pekee. Kuna wakazi wapatao 130,000.

Historia

hariri

Ni mji wa kale sana: ulikuwepo tayari zamani za utawala wa Dola la Roma katika Uingereza ukaitwa Eboracum.

Waviking waliovamia sehemu hii ya Uingereza katika karne ya 9 wakaita mahali "Jorvik" iliyomaanisha "bandari ya chifu" katika lugha yao.

Baada ya uvamizi wa Wanormani katika karne ya 11 polepole matamshi ya jina la Kinormani yakawa "York".

Hadi leo mji una nyumba nyingi za kihistoria.

Jengo kuu ni kanisa kuu maarufu la Anglikana lililokamilishwa mwaka 1472.

Askofu Mkuu wa York ana nafasi ya pili ya kiheshima ndani ya Kanisa Anglikana la Uingereza.

Tangu mwaka 2005 John Sentamu mwenyeji wa Uganda amekuwa askofu mkuu.

Kando ya mji wa kihistoria kuna maeneo ya Chuo Kikuu cha York kilichoanzishwa mwaka 1963.

Vivutio

hariri

York katika nchi ya Uingereza ni mji wa kupendeza sana kutokana na vivutio vilivyoko. Unapotembea mjini York, utafurahishwa na mahali kama:

The Shambles

hariri

The Shambles ni vijia vidogo vidogo vilivyoko mkabala na manyumba mengi. Kivutio hiki hunoga maana ni kizee sana ikitajika kwamba kilianza katika karne ya 14.

York Minster

hariri

Ziara ya York haitafana kama hutaingia katika York Minster, kivutio kingine kilichonoga sana.York Minster ni kanisa lililojengwa kwa uhandisi wa hali ya juu zaidi. Linaoenakana kuwa ilitumika ubunifu na usanii mwingi ili lisimamishwe pahala lipo.

National Railway Museum

hariri

Ziara yako ya York itapendeza zaidi unapotembea na kuona National Railway Museum. Imesemekana kwamba hamna reli nyingine iliyojengwa kwa ustadi mwingi kama National Railywa Museum. Hii ni kwa sababu teknolojia nzuri na za kisasa zimetumika ili isimame mahala ipo.

Viungo vya Nje

hariri
  1. Things to do in York