Nikodemo
Mandhari
Nikodemo (kwa Kigiriki Νικόδημος, Nikodemos) alikuwa mwalimu wa Torati wa madhehebu ya Mafarisayo tena mwanabaraza wa Baraza la Israeli katika karne ya 1 BK.
Anaheshimiwa na Wakristo wengi kama mtakatifu, ingawa sikukuu yake inaadhimishwa katika tarehe tofautitofauti, hasa tarehe 31 Agosti[1].
Nikodemo katika Injili
[hariri | hariri chanzo]Anajulikana kwa sababu ya kutajwa mara kadhaa katika Injili ya Yohane,[2] kama mtu aliyevutiwa na Yesu Kristo ingawa aliogopa maneno ya Wayahudi wenzake.
Ndiyo sababu alimtembelea usiku ili kumuuliza maswali ya dini yao bila kujulikana (Yoh 3:1–21).
Baadaye katika baraza alimtetea Yesu kwamba si haki kuhukumu mtu bila kumsikiliza kwanza, lakini alinyamazishwa (Yoh 7:50–51).
Hatimaye alimsaidia Yosefu wa Arimataya kumzika Yesu (Yoh 19:39–42)[3].
Nikodemo katika picha
[hariri | hariri chanzo]-
Nicodemus (left) talking to Jesus, by Henry Ossawa Tanner
-
Christus und Nicodemus, by Fritz von Uhde (1848–1911)
-
Entombment, by Tizian
-
Jesus and Nicodemus by Crijn Hendricksz, 1616–1645
-
Cima da Conegliano, Nicodemus with Christ's body, Apostle John on the right and Mary to left.
-
Entombment, by Pietro Perugino, with Nicodemus and Joseph from Arimatea
-
Nicodemus (right) talking to Jesus, by William Brassey Hole, (1846–1917)
-
Tanner - Nicodemus coming to Christ II
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Driscoll, James F. "Nicodemus." The Catholic Encyclopedia. Vol. 11. New York: Robert Appleton Company, 1911. 13 Dec. 2014.
- ↑ , aliyetarajia Ufalme wa Mungu uliotangazwa na Yesu, alichukua jukumu la kumzika
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Cornel Heinsdorff: Christus, Nikodemus und die Samaritanerin bei Juvencus. Mit einem Anhang zur lateinischen Evangelienvorlage (= Untersuchungen zur antiken Literatur und Geschichte, Bd.67), Berlin/New York 2003
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Jewish Encyclopedia: Nicodemus
- "St. Nicodemus", Butler's Lives of the Saints
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nikodemo kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |