Mtaguso wa Vienne
Sehemu ya mfululizo kuhusu |
Mitaguso mikuu ya Kanisa Katoliki |
---|
Mtangulizi (50 hivi) |
Roma ya Kale (325–451) |
Mwanzoni mwa Karne za Kati (553–870) |
Mwishoni mwa Karne za Kati (1122–1517) |
Nyakati za uvumbuzi mwingi (1545–) |
Mtaguso wa Vienne (1311-1312) unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na tano.
Mazingira ya kihistoria
[hariri | hariri chanzo]Mtaguso huu ulifanyika Vienne (Ufaransa) baada ya mashindano kati ya Papa Boniface VIII (1294-1303) na mfalme wa Ufaransa Filipo IV.
Hatimaye mwaka 1309 mwandamizi wake, Papa Klementi V (1305-1314), alikubali kubaki Avignon (leo nchini Ufaransa) karibu na himaya ya mfalme huyo. Mapapa walibaki huko hadi mwaka 1377, waliporudi Roma.
Kwa shinikizo la mfalme, Papa alitoa hati Regnans in excelsis (12 Agosti 1308) ili kuitisha mtaguso mkuu huko Vienne tarehe 1 Novemba 1310, kwa lengo la kujadili mada 4:
- suala la Wahekalu;
- vita vya msalaba;
- hali ya imani na Kanisa kwa jumla;
- urekebisho wa Kanisa.
Mtaguso wenyewe na maamuzi yake
[hariri | hariri chanzo]Mtaguso ulichelewa kuanza hadi tarehe 16 Oktoba 1311, walipokuwepo washiriki 170 hivi, ambao kati yao Wafaransa walikuwa zaidi ya thuluthi moja. Wengine walizuiwa na mfalme wa Ufaransa.
Vikao rasmi vikawa vitatu hadi Machi 1312.
Suala la Wahekalu
[hariri | hariri chanzo]Mtaguso uliamua kufuta shirika lao kama alivyopenda mfalme, bila ya kulifanyia utafiti wala kulitolea hukumu.
Suala la Vita vya msalaba
[hariri | hariri chanzo]Mtaguso uliamua kuvianza upya na kwa ajili hiyo kutoza zaka kwa miaka sita, lakini mfalme alijitwalia hizo pesa bila ya kutekeleza ahadi yake ya kuongoza vita hivyo.
Suala la imani
[hariri | hariri chanzo]Mtaguso ulijadili baadhi ya mafundisho hasa ya makundi kadhaa ya watawa, lakini uamuzi ulichukuliwa baadaye tu.
Suala la urekebisho
[hariri | hariri chanzo]Mtaguso ulidai haki za Kanisa ziheshimiwe na serikali za nchi. Pia ulijadili kirefu mahusiano ya ndani, hasa kati ya maaskofu, maparoko na watawa.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Muhtasari wa mtaguso pamoja na matini ya hati ulizozitoa Archived 2 Aprili 2006 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtaguso wa Vienne kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |