Odisei
Odisei (ing. Odyssey) ni utenzi wa kale unaosimulia safari ya ajabu ya mfalme Odiseo wa kisiwa cha Ithaka wakati wa kurudi kutoka vita ya Troia.
Ni kati ya mifano ya kale zadi ya fasihi ya Ugiriki ya Kale ikiaminiwa iliyotungwa na mshairi mashuhuri Homeri takriban mnamo mwaka 1000 KK na kuandikwa mara ya kwamna mnamo 800 KK.
Masimulizi ya utenzi yanaanza baada ya vita ya Troia ambako Odiseo alikuwa mshiriki muhimu aliyehakikisha ushindi wa Wagiriki kwa mbinu wake wa kutumia "Farasi wa ubao".
Safari yake ya kurudi kutoka pwani ya Asia Ndogo hadi upande wa magharibi wa Ugiriki ilikuwa na matatizo mengi ikachukua miaka kumi. Odiseo na wenzake walipaswa kupambana na vizuizi, madubwana na maadui wengi. Wakati huohuo utenzi unasimulia jinsi gani mke wake mwaminifu Penelope anasumbuliwa kwao Ithaka na wanaume wanaoamini Odiseo amekufa hivyo yeye ni mjane anayepaswa kuolewa upya akijitahidi kukataa. Mwanawe Telemachos anajaribu kumtafuta baba.
Baada ya matatizo mengi Odiseo anarudi nyumbani kwako akijionyesha kuwa mwaombaomba asiyetambuliwa na wenyeji. Amakutana na mwanawe Telemachos anakitambulisha kwake. Kwa pamoja wanaamua kuwafukuza na kuwauua wanaume wote waliofika kumwoa Penelope na kuwa mfalme wa Ithaka. Odiseo anajitokeza kama mgombea na kuwashinda wote. Hatimaye anamwambia Penelope yeye niye mumewe akisitasita anamwambia siri ya kitanda chao alichowahi kutengeneza mwenyewe.
Mwishoni wenyeji wa Ithaka wanakubali kwa msaada wa mungu Athena ya kwamba mfalme wao amerudi na amani inarudishwa kisiwani.