Nenda kwa yaliyomo

Onesiforo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Onesiforo katika mchoro mdogo.

Onesiforo (jina la Kigiriki lenye maana ya "mleta faida") alikuwa mwanamume Mkristo wa karne ya 1 aliyetajwa na Mtume Paulo kwa shukrani katika Waraka wa pili kwa Timotheo 1:16-18.

Sababu ni kwamba alimsaidia sana alipokuwa Efeso, halafu akamfuata hadi Roma mpaka akafaulu kumuona na kumfariji bila kuonea aibu minyororo yake.[1][2][3]

Kwa hiyo Paulo alimtakia huruma ya Mungu pamoja na familia yake.[4]

Inasemekana Onesiforo alipata kuwa askofu wa Kolofon (Asia Ndogo), halafu wa Korintho. Hatimaye alifia dini mjini Parium (karibu na Efeso)[5].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Septemba[6][7] au kesho yake[8].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Onesiphorus. The Columbia Encyclopedia, Sixth Edition. 2001-07". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-02-09. Iliwekwa mnamo 2016-07-13.
  2. "...for he often refreshed me and was not ashamed of my chain" 2 Tim:1:16Onesiphorus is contrasted with the other Christians in Asia who have deserted Paul at this time.
  3. "Rutherford, John. "Onesiphorus", ''The International Standard Bible Encyclopedia''". Searchgodsword.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-11-08. Iliwekwa mnamo 2013-09-03.
  4. Because Paul speaks of Onesiphorus only in the past tense, wishes blessings upon his house (family), and mercy for him "in that day", some scholars believe that Onesiphorus had at this point died. Towards the end of the same letter, in 2 Timothy:4:19, Paul sends greetings to "Prisca and Aquila, and the house of Onesiphorus", again apparently distinguishing the situation of Onesiphorus from that of the still living Prisca and Aquila. Paul's reference to Onesiphorus, along with 2 Maccabees:12:40-46, is cited by Catholics as one of the early examples of prayer for the dead,{{cite web|url=http://www.newadvent.org/cathen/04653a.htm |title=Toner, Patrick. "Prayers for the Dead." The Catholic Encyclopedia. Vol. 4. New York: Robert Appleton Company, 1908. 27 Mar. 2013 |publisher=Newadvent.org |date= |accessdate=2013-09-03} while some Protestants opposing this practice reject such an interpretation."Did Paul Pray for the Dead?". ChristianCourier.com. Iliwekwa mnamo 2013-09-03.
  5. "Vailhé, Siméon. "Parium." The Catholic Encyclopedia. Vol. 11. New York: Robert Appleton Company, 1911. 27 Mar. 2013". Newadvent.org. 1911-02-01. Iliwekwa mnamo 2013-09-03.
  6. Martyrologium Romanum
  7. St. Onesiphorus, Catholic Online, iliwekwa mnamo 2016-07-01
  8. "Apostle Onesiphorus of the Seventy, Orthodox Church in America". Oca.org. Iliwekwa mnamo 2013-09-03.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Onesiforo kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.