Jimbo kuu
Mandhari
Jimbo kuu ni jimbo yenye hadhi ya juu upande wa sheria za Kanisa kwa msingi wa historia, wingi wa watu au waamini n.k.
Kwa kawaida lina majimbo ya kandokando chini yake.
Katika Kanisa Katoliki
[hariri | hariri chanzo]Askofu anayeongoza jimbo la namna hiyo anaitwa Askofu mkuu.
Katika Kanisa Katoliki anavaa shingoni nguo maalumu inayoitwa "pallium" kama Papa, kumaanisha kwamba anashiriki mamlaka yake ya juu katika kanda ya Kanisa kadiri ya sheria za Kanisa.
Mwaka 2009 duniani kulikuwa na majimbo makuu kabisa 4, majimbo makuu 540 yenye majimbo chini yake na mengine 77 yasiyo na majimbo chini yake.