Hypothyroidism
Hypothyroidism | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Matamshi | |
Kundi Maalumu | Endokrinolojia |
Dalili | Kuwashwa, udhaifu wa misuli, matatizo ya kulala, mapigo ya moyo ya haraka, kushindwa kuhimili joto, kuhara, kupanuka kwa tezi ya dundumio, kupungua kwa uzani[2] |
Miaka ya kawaida inapoanza | > Kuanzia miaka 20–50 [2] |
Visababishi | Upungufu wa iodini , Ugonjwa wa Grave, ugonjwa wa goita yenye vinundu vingi (multinodular goiter), uvimbe usio wa kisaratani unaozalisha homoni nyingi za tezi ya dundumio (toxic adenoma), kuvimba kwa tezi ya dundumio, ulaji uliopitiliza wa iodini, utumiaji mwingi wa homoni ya tezi ya dundumio ya kutengeneza[2] |
Njia ya kuitambua hali hii | Kulingana na dalili na kuthibitishwa na vipimo vya damu[2] |
Utambuzi tofauti | Msongo wa mawazo, kupoteza kumbukumbu, moyo kushindwa kufanya kazi, ugonjwa wa wasiwasi iliyopitiliza[3] |
Kinga | Utiaji madini joto katika chumvi[4] |
Matibabu | Tiba ya radioiodini, utumiaji wa dawa, upasuaji wa tezi ya dundumio[2] |
Idadi ya utokeaji wake | asilmia 1.2% ya watu (Marekani)[5] |
Hyperthyroidism (uzalishaji wa homoni nyingi mno kwenye tezi ya dundumio) ni hali inayotokana na uzalishwaji wa ziada wa homoni ya tezi kutoka kwenye dundumio.[2] Thyrotoxicosis ni hali ya kuwa na kiwango kikubwa cha homoni za tezi ya dundumio kutokana na sababu yoyote na hivyo kujumuisha hyperthyroidism.[2] Baaadhi ya watu, hata hivyo hutumia maneno hayo kumaanisha kitu kimoja.[2] Dalili na na ishara zake hutofautiana kulingana na watu na zinaweza kujumuisha miwasho, udhaifu wa misuli, matatizo ya kulala, mapigo ya moyo ya haraka, kushindwa kuhimili joto, kuhara, kupanuka kwa tezi ya dundumio, utetemekaji wa mikono, na kupungua kwa uzani.[6]
Dalili kwa kawaida si kali sana kwa wazee na kipindi cha ujauzito.[5][7] Utata usio wa kawaida ni uzalishaji wa homoni nyingi kabisa za tezi ya dundomio ambapo iwapo kuna maambukizo hupelekea kwa dalili kuzidi kuwa mbaya kama vile kuchanganyikiwa na kupanda kwa hali joto na mara nyingi husababisha kifo.[2] Kinyume chake ni hypothyroidism, wakati ambapo tezi ya dundumio haizalishi homoni za kutosha za tezi ya dundumio.[2][8]
Ugonjwa wa Grave ni kisababishi cha takribani asilimia 50% hadi 80% ya visa vyote vya hyperthyroidism nchini Marekani.[2] Visababishi vingine vinajumuisha ugonjwa wa goita yenye vinundu vingi (multinodular goiter), uvimbe usio wa kisaratani unaozalisha homoni nyingi za tezi ya dundumio (toxic adenoma), kuvimba kwa tezi ya dundumio, ulaji uliopitiliza wa iodini na utumiaji mwingi wa homoni ya tezi ya dundumio ya kutengeneza.[4] Kisababishi kisicho cha kawaida ni uvimbe usio wa kisaratani katika tezi ya pituitari.[2] Utambuzi huo unaweza kugunduliwa kwa kuzingatia dalili na ishara na baadaye kuthibitishwa kwa vipimo vya damu.[2] Kwa kawaida vipimo vya damu huonesha kiwango cha chini cha homoni chochezi za tezi ya dundumio (thyroid stimulating hormone, TSH) na viwango vya juu vya T3 au T4.[2] Upimaji wa utumiaji wa iodini ya mionzi na tezi ya dundumio, uchunguzi wa tezi ya dundumio na kingamwili za TSI kunaweza kusaidia kubaini kisababishi.[2]
Matibabu hutegemea kwa kiasi fulani kisababishi na ukali wa ugonjwa.[2] Kuna chaguo kuu tatu za matibabu: tiba ya mionzi ya iodini, umezaji wa dawa na upasuaji wa tezi ya dundumio.[2] Tiba ya mionzi ya iodini hujumuisha umezaji wa iodini-131 kwenye kinywa ambayo hujikusanya na kuharibu tezi ya dundumio ndani ya wiki au miezi.[5] Hypothyroidism iliyojitokeza hutibiwa kwa kutumia homoni ya tezi za dundumio iliyotengenezwa.Utumiaji wa dawa kama vile vizuizi vya beta vinaweza kudhibiti dalili na matumizi ya dawa za kupunguza tezi ya dundumio kama vile methimazole zinaweza kusaidia watu kwa muda mfupi wakati matibabu mengine yakiendelea kufanya kazi. Upasuaji wa kuondoa tezi ya dundumio ni chaguo jingine la matibabu. Hii inaweza kutumika kwa wale wenye vimbe kubwa sana za tezi ya dundumio au wakati saratani inapotiliwa shaka. Nchini Marekani, hyperthyroidism huathiri takriban asilimia 1.2% ya idadi ya watu wote.[5] Hutokea kati ya mara mbili hadi kumi zaidi kwa wanawake.[2] Watu zaidi ya umri wa miaka 60 huathiriwa zaidi.[2] Kwa kawaida, huanza kati ya umri wa miaka 20 hadi 50.[9] Kwa ujumla ugonjwa huu huwapata zaidi wale walio na zaidi ya miaka 60.[10]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "hypothyroidism - definition of hypothyroidism in English from the Oxford dictionary". OxfordDictionaries.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-01-10. Iliwekwa mnamo 2016-01-20.
- ↑ 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 2.10 2.11 2.12 2.13 2.14 2.15 2.16 2.17 2.18 "Hypothyroidism". National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. Machi 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 5 Machi 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Ferri, Fred F. (2010). Ferri's differential diagnosis : a practical guide to the differential diagnosis of symptoms, signs, and clinical disorders (tol. la 2nd). Philadelphia, PA: Elsevier/Mosby. uk. Chapter H. ISBN 978-0323076999.
- ↑ 4.0 4.1 Syed S (Aprili 2015). "Iodine and the "near" eradication of cretinism". Pediatrics. 135 (4): 594–6. doi:10.1542/peds.2014-3718. PMID 25825529.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 5.0 5.1 5.2 5.3 Garber JR, Cobin RH, Gharib H, Hennessey JV, Klein I, Mechanick JI, Pessah-Pollack R, Singer PA, Woeber KA (Desemba 2012). "Clinical practice guidelines for hypothyroidism in adults: cosponsored by the American Association of Clinical Endocrinologists and the American Thyroid Association" (PDF). Thyroid. 22 (12): 1200–35. doi:10.1089/thy.2012.0205. PMID 22954017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-01-14. Iliwekwa mnamo 2013-12-25.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Preedy, Victor (2009). Comprehensive Handbook of Iodine Nutritional, Biochemical, Pathological and Therapeutic Aspects. Burlington: Elsevier. uk. 616. ISBN 9780080920863. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-05-18. Iliwekwa mnamo 2020-07-28.
- ↑ Chakera AJ, Pearce SH, Vaidya B (2012). "Treatment for primary hypothyroidism: current approaches and future possibilities". Drug Design, Development and Therapy (Review). 6: 1–11. doi:10.2147/DDDT.S12894. PMC 3267517. PMID 22291465.
{{cite journal}}
: CS1 maint: unflagged free DOI (link) - ↑ Persani L (Septemba 2012). "Clinical review: Central hypothyroidism: pathogenic, diagnostic, and therapeutic challenges". The Journal of Clinical Endocrinology and Metabolism (Review). 97 (9): 3068–78. doi:10.1210/jc.2012-1616. PMID 22851492.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Hypothyroidism". Merck Veterinary Manual, 10th edition (online version). 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-08-23. Iliwekwa mnamo 2013-12-25.
- ↑ Mosby's Medical Dictionary (tol. la 9). Elsevier Health Sciences. 2013. uk. 887. ISBN 9780323112581. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-07.