Historia ya Yemen
Historia ya Yemen inahusu eneo ambalo leo linaunda jamhuri ya Yemen.
Hadi mwaka 1990 palikuwa na nchi mbili za Yemen Kaskazini na Yemen Kusini.
Ile ya kaskazini ilikuwa Ufalme wa Yemen baada ya Imamu Yahya Muhamad wa kundi la Zaidiya kuvamia velayat ya Yemen ya milki ya Waturuki Waosmani (1 Novemba 1918). Baadaye ikawa Jamhuri kwa njia ya mapinduzi (1962).
Ile ya kusini ilikuwa kwa sehemu (Aden) koloni na kwa sehemu (Hadramaut) nchi lindwa ya Waingereza. Baada ya ukoloni kwisha ikawa mara moja Jamhuri (30 Novemba 1967).
Nchi hizo mbili ziliungana tarehe 22 Mei 1990, lakini uongozi ulizidisha ufisadi, na tangu mwaka 2011 hali ya siasa ni tata. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaendelea kwa misaada kutoka nchi za nje, hasa kutokana na uwepo wa makundi makubwa adui ya Wasuni na Washia.
Matokeo yake ni njaa kwa wakazi 17,000,000 kiasi kwamba Yemen imehesabika kuwa nchi inayohitaji zaidi misaada ya kibinadamu.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Yemen kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |