Konstantinos Filippidis
Konstantinos Filippidis (kwa Kigiriki: Κωνσταντίνος Φιλιππίδης; alizaliwa Athene, novemba 1986) ni mruka upondo wa Ugiriki. Alishinda medali ya dhahabu kwenye michuano ya ndani ya dunia 2014 na medali ya fedha kwenye michuano ya ulaya 2017.alishika nafasi ya sita kwenye michezo ya olimpiki 2012 huko London.
Akiwa mdogo
[hariri | hariri chanzo]Alifanikiwa kwenye ngazi ya vijana,akamaliza wa tano kwenye michuano ya vijana ya duna 2003 na michuano ya vijana ya Dunia 2004 na kushinda medali ya fedha kwenye michuano ya majira ya joto ya vijana 2005. Mwaka huo huo alishinda medali ya fedha kwenye michuano ya majina ya joto ya Universiade 2005 kwa urukaji bora binafsi wa mita 5.75. Alishindana pia kwenye michuano ya dunia 2005 na michuano ya riadha ya ulaya 2006 bila kufuzu kwa fainali.
kusimamishwa 2007-09
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2007 Filippidis alikutwa na tuhuma za utumiaji wa madawa ya kulevya ya etilephrine. Sampuli ililetwa juni 16 2007 kwenye upimaji wa kwenye mashindano katika michuano ya riadha ya taifa. Alisimamishwa na Shirikisho la kimataifa la vyama vya riadha (IAAF) kuanzia julai 2007 hadi julai 2009. Alifanikiwa kuomba kupunguziwa kupindi chake cha kutostahiki, akakubaliwa na baadaye alistahiki kuendelea na mashindano kuanzia februari 16 2009.[1]
Kurudi 2010 2012
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kurudi mwaka 2009, aliboresha ubora wake na rekodi ya taifa ya ndani (5.70 m) na baadae akashika nafasi ya 4 kwenye michuano ya ndani ya dunia 2010
Mwaka unaofuata alianza msimu kwa rekodi nyingine ya ndani (5.70 m) na pia akafika fainali ya michuano ya Ulaya cha ndani 2011, akishika nafasi ya 5. Durind kipindi cha majira ya joto alishika nafasi ya 3 kwenye ligi ya Almasi ya Shirikisho la kimataifa la vyama vya riadha (IAAF) huko Paris kwa mita 5.68, nafasi ya pili kwa mita 5.72 katika mkutano huko Jockgrim na akashinda ubingwa wa taifa wa Ugiriki kwa urukaji wa mita 5.73. Katika michuano ya dunia 2011,aliboresha ubora wa msimu wake na akachukua nafasi ya 6 kwa urukaji wa mita 5.75, ukilingana na rekodi yake ya Ugiriki ya 2005.[2]
Kwenye msimu wa ndani 2012, Filippidis alivunja tena rekodi ya taifa ya Ugiriki kwa urukaji wa mita 5.75 wakati huo huo kwenye michuano ya dunia ya ndani ya Shirikisho la kimataifa la vyama vya riadha (IAAF) 2012 huko Istanbul alifika fainali akichukua nafasi ya 7.Baadaye katika kipindi cha joto,alikuwa tena wa saba kwenye fainali ya olimpiki ya majira ya joto huko London. Baada ya michezo, aliboresha mara mbili rekodi ya Ugiriki (kwanza mpaka mita 5.76 na mwisho mpaka mita 5.80)
Michuano ya ndani ya Dunia
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2013 Filippídis alichukua nafasi ya kwanza kwenye World Challenge huko Berlin.aliweza kuruka wa mita 5.70 kwenye jaribio lake ya 3.
Konstantinos Filippídis alichukua nafasi ya kwanza kwenye michuano ya ndani ya dunia 2014 huko Sopot. Bingwa wa Ugiriki aliendelea mpaka fainali yote bila kushindwa mpaka ushindi wa urefu wa mita 5.80 akashinda akashinda ubingwa wa dunia na mrukaji bora wa msimu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "14 September 2007 • The Holy Cross". Homily Service. 40 (10): 26–29. 2007-08-16. doi:10.1080/07321870701454095. ISSN 0732-1872.
- ↑ Instone, Stephen (2015-12-22), "athletics, Greek", Oxford Research Encyclopedia of Classics, Oxford University Press, iliwekwa mnamo 2021-10-05