Juja
Juja ni mji upatikanao katika kaunti ya Kiambu, kati ya nchi ya Kenya. Mji huu uko katika umbali wa kilometa 36 Kaskazini Mashariki mwa Jiji la Nairobi. Ni kata ya eneo bunge la Juja[1].
Mji una wakazi 40,446 (sensa ya mwaka 2009[2]).
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Juja ina au mwinuko urefu wa kilometa 700 kutoka juu ya bahari. katika ramani ya dunia, Juja hupatikana katika longitude ya 37 07' 00" na latitude ya -1 11' 00".[3]
Hali ya hewa
[hariri | hariri chanzo]Kulingana na ripoti kutoka kituo cha utafiti wa hali ya hewa cha Nairobi/Wilson kilichoko umbali wa kilometa 74.8, mji wa Juja una kiwango cha joto cha Nyuzi 24. Upepo huvuma kwa kiwango cha kilometa 23 kwa saa ukielekea Kaskazini Mashariki.
Pia kuna mawingu mepesi katika umbali wa takribani futi 2600 juu ya ardhi.
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Mji wa Juja una taasisi mbalimbali za elimu kuanzia Shule za Msingi, Shule za upili na Vyuo vikuu.
Miongoni mwa taasisi za mafunzo ambazo zimeupa mji wa Juja umaarufu mkubwa ni chuo kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta, ambacho kinapatikana huko mjini.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Electoral Commission of Kenya: Registered voters per polling station by electoral area/ward and constituency Archived Septemba 29, 2007, at the Wayback Machine
- ↑ http://www.citypopulation.de/search_d.html?q=Juja%20%22karten%22
- ↑ http://www.tageo.com/index-e-ke-v-01-d-m3102515.htm Satelite view of Juja
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Ramani ya Juja
- JUJA CNTRAL KENYA geography population Map cities coordinates location
- Picha ya Setilaiti ya Juja Kwa Hisani ya Google Satelite
- Kuhusu Eneo Bunge la Juja Archived 7 Agosti 2010 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Juja kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |