Nenda kwa yaliyomo

Dawa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Duka la Dawa
Duka la Dawa muhimu

Dawa (kwa Kiingereza drug) ni dutu lolote -kama si chakula- ambalo linabadilisha hali ya mwili au ya roho ya mtu baada ya kuingizwa mwilini mwake.

Njia za kuingiza dawa mwilini ni pamoja na mdomo, pua, ngozi au sindano.

Kuna madawa asilia yanayoundwa kutokana na mimea na mengine sintetiki (yaani yaliyotengenezwa kwa njia ya kikemia).

Mara nyingi dawa hutumiwa na binadamu kwa makusudi. Yanamezwa, kupakiwa au kudungwa kwa sindano. Kuna pia madawa yanayoweza kuathiri watu yakiwafikia bila kukusudi, mfano kwa kuliwa bila kujua au kutokana na usambazaji wa dawa hewani au kwenye maji kwa mfano baada ya moto mkubwa au ajali.

Aina za madawa

[hariri | hariri chanzo]
  • Madawa mengi yanayotumiwa na watu hutengenezwa kama madawa ya tiba. Mifano ni aspirin au paracetamol. Ni madawa ambayo yanaagizwa na tabibu dhidi ya ugonjwa fulani. Kusudi ni kutibu, kuponya, kuzuia au kutambua ugonjwa au pia kuimarisha afya. Dawa za famasia zinaweza kutumika kwa muda tu au mara kwa mara katika maradhi yasiyoponyeka.
  • Madawa mengine hupatikana ndani ya mimea au pia wanyama kadhaa. Tangu kale athira zao zilijulikana kwa watu na elimu yao kukusanywa na wataalamu wa kienyeji na kutumiwa kwa tiba au pia kama sumu. Madawa haya hujulikana pia kwa jina la mitishamba. Hadi leo majani, mizizi au sehemu nyingine za mimea hukusanywa kwa utengenezaji wa madawa ya tiba.
  • Madawa mengine yanajulikana kuathiri hali ya kiroho kwa njia inayotafutwa na watumiaji.
    • Madawa ya raha kama kafeini ya kahawa au chai na nikotini ya tumbaku yanakubaliwa kwa kiasi kikubwa katika jamii.
    • Madawa ya kulevya, kama vile heroini, ni madawa yanayoweza kusababisha ulevi, mara nyingi pamoja na hali ya uraibu ambako mtumiaji anaanza kutegemea dawa hili hadi hawezi kuiacha tena. Kutokana na hatari kwa afya zinazokuja na matumizi madawa haya yamepigwa marufuku katika nchi nyingi.
  • Madawa ya tiba ya wanyama: ilhali wanyama wengi hasa mamalia wanafanana kimaumbile na binadamu madawa mengine hutumiwa pia kutibu maradhi ya wanyama.
  • Madawa ya kilimo ni hasa madawa ya kuua au kuzuia wadudu mashambani au pia kuua au kuzuia upanuzi wa fungi na vijidudu vinavyosababisha maradhi ya mimea. Mara nyingi zinafanya kazi ya sumu na kutokana na hatari ya mabaki yao kwenye mazao ya chakula kwa binadamu kuna jitihada nyingi kutumia dawa za kibiolojia katika kilimo.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dawa kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.