UNESCO
wakala maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa elimu, sayansi na utamaduni
UNESCO ni kifupisho cha United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization yaani Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa.
Ni kitengo cha Umoja wa Mataifa ambacho kinashughulika habari za elimu, sayansi na utamaduni duniani.
Kisheria UNESCO ni shirika la kujitegemea lenye madola wanachama 191.
Kati ya shughuli muhimu za UNESCO mojawapo ni Orodha la Urithi wa Dunia linalojumlisha mahali penye umuhimu wa pekee kihistoria, kisayansi au kiutamaduni.
Nchi zote zina mahali angalau moja orodhani, nyingine zina pengi, hasa Italia na Hispania.
Viungo vya nje
hariri- Tovuti rasmi kwa Kiingereza
- Tovuti rasmi ya Redio ya UM kwa Kiswahili Archived 5 Februari 2018 at the Wayback Machine.
- Kenya sacred sites listed by Unesco Archived 19 Oktoba 2011 at the Wayback Machine. (online video 15 min)