Nenda kwa yaliyomo

Zimbabwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jamhuri ya Zimbabwe
Republic of Zimbabwe, Africa
Flag of Zimbabwe
(Bendera ya Zimbabwe) (Nembo ya Zimbabwe)
Kaulimbiu ya Taifa Unity, Freedom, Work (Kiingereza: Umoja, Uhuru, Kazi) " |
Wimbo wa Taifa
Location of Zimbabwe
Lugha rasmi Kiingereza na 15 nyingine
Mji Mkuu Harare
Mji mkubwa Harare
Rais Emmerson Mnangagwa
Eneo
 - Jumla
 -Maji
 -Eneo kadiriwa
km² 390,757
1%
ya 60 duniani
Umma
 - Kadirio
 - Sensa,
 - Msongamano wa watu
15,178,979 ya 66 duniani
(2022)
; 32/km²
; ya duniani
Chumo cha uchumi
 - Jumla
 - kwa kipimo cha umma
$24.99 billion (Orotha ya nchi GDP (kidogo))
$2,100 (Orodha ya nchi kulingana na GDP kwa umma)
Uhuru
 - Kadirifu
 - Barabara
(kama Rhodesia) 11 Novemba 1965
(kama Zimbabwe) 18 Aprili 1980
Fedha Dolar ya Marekani|
Saa za Eneo UTC +2
Intaneti TLD .zw
kodi za simu 263

Jamhuri ya Zimbabwe (iliyojulikana wakati wa ukoloni kama Rhodesia ya Kusini) ni nchi isiyo na bahari iliyoko upande wa kusini wa Bara la Afrika, kati ya mto Zambezi na mto Limpopo.

Imepakana na Afrika ya Kusini upande wa kusini, Botswana upande wa magharibi, Zambia upande wa kaskazini-mashariki, na Msumbiji upande wa mashariki.

Jina

Jina Zimbabwe linatokana na neno "dzimba dzamabwe" linalomaanisha "nyumba ya mawe" kwa lugha ya Kishona. Nyumba hiyo ya mawe, ambayo imehifadhiwa kama eneo la kihistoria, ilikuwa makao ya Ufalme wa Mutapa ambaye mfalme wake aliongoza eneo hilo miaka ya kale.

Mikoa ya Zimbabwe.
Pesa ya Zimbabwe hadi 2015, dollar ya Zimbabwe ilipofutwa, na Dolar ya Marekani kufanywa pesa rasmi.

Eneo

Zimbabwe imegawiwa katika mikoa 8 na miji 2 yenye hadhi ya mikoa. Imegawiwa zaidi katika wilaya 59 na kata 1,200.

Mikoa ya Zimbabwe ni:

Miji minne mikubwa ya Zimbabwe ni:

Maporomoko ya maji (Bridal Vei), paa za mashariki
Duka, Paa za mashariki, 1989

Historia

Historia ya awali

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Tangu karne ya 11, Zimbabwe ya leo imekuwa na falme imara kwenye njia muhimu ya biashara, hasa ufalme wa Mutapa.

Ukoloni

Kampuni ya British South Africa ya Cecil Rhodes iliweka mipaka ya sasa katika miaka ya 1890.

Koloni la Uingereza lilianzishwa mwaka 1923 kwa jina la Southern Rhodesia.

Mwaka 1965, serikali ya walowezi Wazungu ilijitangazia uhuru kwa jina la Rhodesia tu.

Baada ya miaka 14 ya kutengwa kimataifa na kupigana na raia Waafrika katika miaka ya 1970, mapatano ya mwaka 1979 yalikubali wakazi wote wawe na haki ya kupiga kura na nchi ikawa huru kweli kwa jina la Zimbabwe mwaka 1980.

Baada ya uhuru

Rais Robert Mugabe alipata umaarufu katika siasa kama mpiganaji dhidi ya ukoloni lakini pia kama aina ya dikteta aliyerudisha nyuma uchumi wa nchi.

Baada ya yeye kulazimishwa na wanajeshi kujiuzulu, tarehe 24 Novemba 2017 Emmerson Mnangagwa amekuwa rais mpya wa Zimbabwe.

Watu

Wakazi wengi (82%) ni wa kabila la Washona, 14% ni Wandebele, 2% ni wa makabila mengine ya Kiafrika, 1% ni machotara, Wahindi, Wazungu n.k.

Kwa sasa lugha rasmi ni 16. Lugha kubwa ni Kishona (70%) na Kindebele (20%). Kiingereza ni lugha ya kwanza ya chini ya asilimia 2.5% za wakazi.

Upande wa dini, 84.1% ni Wakristo (hasa Waanglikana, Wakatoliki 8%, Wasabato na Wamethodisti). Waliobaki ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika (4.5%), ni Waislamu (0.7%), au hawana dini (10.2%) .

Mawasiliano

Mawasiliano ya simu na mitambo yake yanaendeshwa na Tel-One0, kampuni ya serikali.

Kuna kampuni 3 za simu za mikononi: Econet Wireless, Net*One na Telecel.

Tazama pia

Tanbihi


Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Serikali

Habari

Wanamgambo

Maelekezo

Utalii

Nyingine


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Zimbabwe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.