Libya
Libya ni nchi ya Afrika ya Kaskazini kwenye Bahari ya Mediteraneo, inayopakana na Misri, Sudan, Niger, Chad, Algeria na Tunisia.
| |||
Lugha rasmi | Kiarabu | ||
Mji Mkuu | Tripoli | ||
Serikali | Jamhuri ya Kiislamu | ||
Mkuu wa Dola | Mohamed al-Menfi | ||
Waziri Mkuu | Abdul Hamid Dbeibeh | ||
Eneo | km² 1.759.541 | ||
Idadi ya Wakazi | 7,054,493 (Julai 2022) | ||
Wakazi kwa km² | 3,74 | ||
JPT/mkazi | 4.293 US-$ (2004) | ||
Uhuru | kutoka Italia tarehe 24 Desemba 1951 | ||
Pesa | Dinari ya Libya | ||
Wakati | UTC+1 | ||
Wimbo la Taifa | "Libya, Libya, Libya" | ||
Eneo kubwa la nchi (90%) ni sehemu ya jangwa la Sahara. Chini yake kuna akiba kubwa ya petroli, ambayo ndiyo utajiri wa nchi.
Miji mikuu ni Tripoli, Benghazi na Misratah.
Historia
haririWakazi asili walikuwa Waberber. Baadaye wakaja Wafoinike upande wa magharibi na Wagiriki upande wa mashariki.
Hatimaye Libya ikamezwa na Dola la Roma, na Ukristo ukaenea.
Baada ya dola hilo kuanguka, Wavandali waliteka sehemu kubwa ya nchi.
Katika karne ya 7 Waarabu waliingiza Uislamu na utamaduni wao.
Mwaka 1551 Waturuki walifukuza Wazungu kutoka Tripoli wakatawala hadi karne ya 20.
Nchi ilitawaliwa na Waitalia tangu mwaka 1911 hadi 1941 ilipotekwa na Waingereza ambao, baada ya Vita vikuu vya pili kwisha, waliacha nchi mwaka 1951 mikononi mwa mfalme mwenyeji, Idris I, aliyekuwa amepinga ukoloni tangu mwaka 1920 (Vita vya Libya dhidi ya Italia).
Kisha kumpindua mfalme huyo, Muammar al-Gaddafi alitawala kidikteta tangu mwaka 1969 hadi alipopinduliwa na kuuawa mwaka 2011 kwa mkono wa N.A.T.O.
Baada ya hapo wananchi wanazidi kupigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mwaka 2020 kulikuwa na makubaliano ya kusimamisha vita na kuunda serikali ya pamoja ili kuandaa uchaguzi mkuu.
Watu
haririWakazi wa Libya ni hasa mchanganyiko wa Waberberi, Waarabu na Waturuki (74%), mbali na Waberberi (25%) ambao ndio wakazi asilia, lakini wengi wao wameanza kutumia lugha ya Kiarabu pia. Kuna pia wahamiaji kutoka nchi za jirani, za kandokando ya Bahari ya Kati na kutoka Bara Hindi.
Wakazi wameongezeka tangu mwaka 1970 kutoka milioni 2.5 hadi kuwa karibu milioni 7 mwaka 2022. Nusu ya wakazi wote ni vijana chini ya umri wa miaka 16. Sehemu kubwa kabisa (80%) huishi sehemu za pwani.
Lugha kuu ni Kiarabu pamoja na lugha kadhaa za Kiberberi. Ndizo:
- Kinafusi (wasemaji 101.000)
- Kighadames (wasemaji 42.000)
- Kitamascheq (Tuareg; wasemaji 17.000)
Upande wa dini, unatawala Uislamu (97%). Wakristo ni zaidi ya 100,000, wakiwemo hasa Wakopti (60,000) na Wakatoliki (40,000).
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- Libya entry at The World Factbook
- Libya katika Open Directory Project
- Libya profile from the BBC News.
- Wikimedia Atlas of Libya
- [1]
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Libya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |