Demokrasia ya moja kwa moja
Demokrasia ya moja kwa moja ni aina ya demokrasia ambayo wananchi wote wanaweza kushiriki katika kuamua masuala ya kisiasa, kijamii, kisheria, na kiuchumi bila kutumia chombo cha uwakilishi kama vile bunge.
Uwezo huu wa wananchi kutoa maamuzi unaweza kuwapa wananchi hata uwezo wa kimahakama ingawa mara nyingi wananchi hupewa uwezo wa kutunga au kupitisha sheria tu.
Muundo wa demokrasia ya asili uwezo huu wa kutunga au kupitisha sheria na kupitisha maamuzi ulikuwa uko mikononi mwa wananchi wenyewe na sio wawakilishi wao. Kutegemeana na mfumo wenyewe wa demokrasia ya moja kwa moja, wananchi huwa wana uwezo wa kutunga sheria, kupitisha sera, kuwaweka madarakani na pia kuwaondoa madarakani viongozi.
Demokrasia ya moja kwa moja ni tofauti na demokrasia inayofuatwa katika nchi nyingi duniani hivi sasa ambapo wananchi huchagua wawakilishi wao katika uchaguzi.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |