Dwight D. Eisenhower
Dwight David Eisenhower (14 Oktoba 1890 – 28 Machi 1969) alikuwa mwanajeshi na mwanasiasa kutoka nchi ya Marekani. Watu wengi walikuwa humwita Ike (tamka Aik). Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia alikuwa jenerali mkuu aliyeongoza uvamizi wa Normandy tarehe 5 Juni 1944. Kuanzia mwaka wa 1953 hadi 1961 alikuwa Rais wa 34 wa Marekani. Kaimu Rais wake alikuwa Richard Nixon.
Dwight D. Eisenhower | |
Dwight D. Eisenhower mnamo Mei 1959 | |
Makamu wa Rais | Richard Nixon |
---|---|
mtangulizi | Harry S. Truman |
aliyemfuata | John F. Kennedy |
tarehe ya kuzaliwa | Denison, Texas, Marekani | Oktoba 14, 1890
tarehe ya kufa | 28 Machi 1969 (umri 78) Washington, D.C., Marekani |
mahali pa kuzikiwa | Dwight D. Eisenhower Presidential Library, Museum and Boyhood Home |
ndoa | Mamie Eisenhower (m. 1916) |
watoto |
|
mhitimu wa | United States Military Academy |
signature | |
Military service | |
Awards |
Maisha
haririDwight Eisenhower alizaliwa tarehe 14 Oktoba, mwaka wa 1890, kama mtoto wa tatu wa David na Ida Eisenhower katika mji wa Denison, Texas. Watoto wote saba walikuwa wavulana, majina yao: Arthur, Edgar, Dwight, Roy, Paul (aliyefariki utotoni na dondakoo), Earl, na Milton. Kabla Dwight hajafikisha umri wa mwaka mmoja, wazazi wake walihamia mji wa Abilene, Kansas, ambapo alilelewa na kuhitimu shule. Baada ya kufanya kazi mbalimbali za mikono, alifaulu mtihani wa kuingia chuo cha kijeshi cha Westpoint ambapo alihitimu mwaka wa 1915.
Tarehe 1 Julai 1916, alifunga ndoa na Mamie Geneva Doud. Mtoto wao wa kwanza alizaliwa tarehe 23 Septemba 1917, jina lake Doud Dwight Eisenhower lakini aliitwa Icky na wote. Alifariki na homa ya vipele vyekundu tarehe 2 Januari 1921, akiwa na miaka mitatu tu. Mtoto wa pili, John Sheldon Eisenhower, alizaliwa mwaka wa 1922.
Eisenhower alihamishwa kikazi mahali mbalimbali siyo Marekani tu lakini pia nje, k.m. Panama na Ufaransa. Mara nyingi alifanya kazi ya ofisi ingawa alipendelea kazi ya kijeshi yenyewe. Nafasi yake alifika wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Kuanzia mwaka wa 1942, Eisenhower alikuwa kamanda, kwanza upande wa Afrika Kaskazini, akiwa na makao makuu mjini Algiers, halafu aliongoza uvamizi wa Italia, na mwishoni alitayarisha uvamizi wa Normandy tarehe 5 Juni 1944.
Baada ya vita alikuwa kamanda mkuu wa NATO. Watu wengi wa Chama cha Republican walimpendelea agombee urais mwaka wa 1952, yeye lakini hakutaka kuingia mambo ya siasa. Hata hivyo aliandikishwa na kuwa mgombea wa Repulican. Baada ya kumshinda Adlai Stevenson III, Eisenhower alikuwa Rais wa Marekani kwa awamo mbili hadi 1961. Wakati wa urais wake, vita ya Korea ilikomeshwa. Pia, siasa ya Marekani iliathiriwa na mawazo dhidi ya Wakomunisti yaliyotekelezwa na Joseph McCarthy.
Baada ya kustaafu, Eisenhower alikaa pamoja na mke wake katika mji wa Gettysburg, Pennsylvania. Tarehe 28 Machi 1969, alifariki hospitalini baada ya kupatwa na shtuko la moyo.
Marejeo
haririPinkley, Virgil. 1979. Eisenhower Declassified. Old Tappan: Fleming Revell.
Tazamia pia
hariri}}