Baghdad (Kar.: بغداد‎ ​) ni mji mkuu pia mji mkubwa nchini Iraq. Iko kando la mto Tigris.

Muonekano wa jiji la Baghdad, Machi 2017


Jiji la Baghdad
Nchi Iraq

Baghdad iliundwa na Waarabu badala ya mji mkuu wa kale Ktesiphon katika karne ya 8. Ilikuwa mji mkuu wa dunia ya Uislamu wakati wa ukhalifa wa Abbasiyya. Mwaka 1258 mji uliharibiwa na jeshi la Mongolia.

Baadaye ilikuwa makao makuu ya utawala wa Mesopotamia katika Dola la Uturuki. Tangu 1921 ilitawaliwa na Uingereza pamoja na Iraq yote. Tangu 1936 ilikua mji mkuu wa Iraq kama nchi ya kujitegemea.

Mji uliharibiwa na Vita ya Ghuba na vita ya wenyewe kwa wenywe nchini Iraq.

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Baghdad kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: